2014-01-24 15:24:17

Mahakama ya Rota yazindua mwaka mpya wa kazi


Mahakama ya Kitume inayojulikana kwa jina la Rota Romana, Ijumaa hii imekuwa na mkutano wake kwa ajili ya kuzindua mwaka mpya wa kazi .
Baba Mtakatifu Francisko, akiwahutubia wajumbe wa mkutnao huu ,aliitumia nafasi hiyo kutoa shukurani zake za dhati kwa huduma na mchango wao mkubwa kwa Kanisa. Na hasa kwa wanasheria katika idara hii ya Rota, wanaofanya kazi kwa niaba na mamlaka ya mrithi wa Petro.

Papa ameeleza, mwelekeo wa kisheria na mwelekeo wa huduma ya kichungaji kwa Kanisa si mambo mawili pinzani, kwa sababu, vyote huchangia mafanikio ya lengo na umoja wa hatua sahihi kwa Kanisa. Shughuli ya mahakama ya Kanisa , ambayo huunda huduma kwa kweli katika haki, ina maana kubwa kwa wachungaji , kwa sababu ni ufuatiliaji mzuri kwa waamini na ujenzi wa jumuiya ya kikristo iliyo imara katika imani. Shughuli hii endelevu ni maendeleo na nguvu ya kipekee katika utawala bora, na huduma ya kiroho kwa watu wa Mungu , na hiyvo kikamilifu imeingizwa katika njia za utume wa Kanisa.
Papa ameendelea kuitaja mahakama ya kitume kuwa ni ushiriki halisi katika huduma kwa watu wa Mungu katika mtazamo wa kuimarishaji ushirika kamili kati ya muumini kama mtu binafsi, na kati ya wengine kama mwili mmoja wa kanisa.

Papa pia ametoa mchango wake katika mada za mkutano huo, akianza na ukomavu kibinadamu kwamba, Mahakama anahitajika ukomavu, unaoweza kuonenyeshwa na utulivu wakati wa kutoa hukumu, na maoni ya mtu binafsi. Na katika uwezo wa akili na matarajio halali ya jamii inayohudumiwa, kama inavyoelezwa katika tafasiri ya hati ya “Anumus Communitatis”, inayoonyesha nafasi ya taifa la Mungu katika mwelekeo wa utendaji wake wa kazi na katika kufanikisha haki si tu kama utendaji wa mkono wa sheria na zahania, lakini kama hitaji msingi la kweli. Na matokeo yake hayatategemei tu kuridhika na ufahamu na habari bandia kutoka kwa watu wanaosubiri hukumu kutolewa, lakini inahitaji kuzama katika kilindi cha tatizo na vipengere vingine vyote muhimu mahakamani.








All the contents on this site are copyrighted ©.