2014-01-24 13:43:45

Jitahidini kuuishi Ubatizo wenu kila siku, kwa kumvaa Kristo!


Wakati huu Wakristo wanapojiandaa kufunga rasmi Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo sanjari na Siku kuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo, mwalimu na mtume wa Mataifa, hapo tarehe 25 Januari 2014.

Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha waamini kwamba, wanashikamanishwa na Kristo kwa njia ya Ubatizo na Fumbo la Msalaba. Katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, Baba mtakatifu anawaalika waamini kuhakikisha kwamba, wanaishi Ubatizo wao kila siku, wakijitahidi kuwa ni viumbe wapya waliozaliwa kwa Maji na Roho Mtakatifu, kiasi cha kumvaa Kristo na kuanza kutembea katika mwanga wa maisha na utu mpya!.







All the contents on this site are copyrighted ©.