2014-01-23 08:14:39

Wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Roma wapongezwa kwa umoja, mshikamano na udugu


Mama Josephine Gaita, Balozi wa Kenya nchini Italia ni kati ya wageni mashuhuri waliohudhuria Ibada ya Fumbo la Ekaristi Takatifu, wakati Mafrateri wa Shirika la Upendo, maarufu kama Rosmini walipokuwa wanapewa Daraja ya Ushemasi mjini Roma, hivi karibuni. Mashemasi hao wapya ni: Fulgence Oisso Epimaki kutoka Tanzania na Shemasi Richard Mwanzia Munyao kutoka Kenya.

Balozi Gaita ambaye yuko nchini Italia kwa kipindi cha miaka mitatu sasa amewapongeza wananchi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuonesha umoja, mshikamano na upendo wa kidugu wakati wa Ibada ya Misa Takatifu. Anasema, alishangazwa kuona umati mkubwa wa Mapadre, Watawa na Waamini walei walioshiriki katika Ibada hii kutoka Afrika Mashariki.

Balozi Gaita amewataka Mashemasi wapya kuwa waaminifu kwa wito na maisha waliojichagulia wenyewe, tayari kumtumikia Mungu na jirani zao bila ya kujibakiza. Kamwe wasikate tamaa kwani kuna Familia ya Mungu kutoka Afrika Mashariki inayowasindikiza katika maisha na utume wao kama Makleri.







All the contents on this site are copyrighted ©.