Jumatano, Papa Francisko mara baada ya kukamilisha Katekesi yake kwa mahujaji na
wageni, aliwaombea viongozi wanaokutana Geneva Uswiss kwa ajili ya kuzungumzia majawabu
yanayoweza kumaliza vita ya Syria. Vita hii ya Syria, imesababisha zaidi ya watu
100 elfu kupoteza maisha na mamillioni wengine kuishi ugenini kama wakimbizi. Mkutano
huu unaojulikana kama Geneva II , ni mkutano wa kimataifa kwa ajili ya amani nchini
Syria, ulifunguliwa Jumatano, Januari 22 , mjini Montreaux , Uswisi na majadiliano
yanaendelea Geneva hadi Ijumaa, Januari 24, na unahudhuriwa na viongozi wa kisiasa,
kidini na wataalam wa sera. Akizungumza mwishoni mwa Katekesi yake, Papa Francisko
alimwomba Bwana aiguse mioyo ya watu wote wanaohusika katika mgogoro huu na pia washiriki
wa mkutano wa Geneva II , ili waweze kutazama tu yaliyo mema kwa watu wa Syria hasa
kwa wakati huu wa majaribu makubwa kwa Wasyria , ili waweze mara moja kukomesha vurugu
na kufikisha mwisho wa vita , ambayo tayari inasababisha mateso makubwa hasa wka
watu wasiokuwa na hatia au uwezo wa kujitetea.
Baba Mtakatifu Francisko alionyesha
tumaini lake kwamba , taifa pendwa la Syria, litapendelea kutembea tena katika njia
ya amani, maridhiano , na ukarabati unaowashirikisha raia wote wa Syria , ili kwamba
kila mmoja aweza kumwona mwingine kuwa si adui , au mpinzani, lakini kama ndugu kuwakaribishwa
na kukumbatiwa. Utume wa Bahari Aidha Papa aliutumia muda
huo wa kutoa katekesi kwa mahujaji na wageni, pia kutoa salaam zake maalum na kuwakaribisha
kwa Waratibu wa Kimkoa wa Utume wa Kichungaji katika ulimwengu wa Bahari, wanaokutana
Rome wiki hii. Katika hotuba yake fupi , Papa Francisko alitoa wito kwa wale wanaofanya
kazi kwa ajili ya ustawi wa mabaharia na familia zao , kuwa sauti ya wale wanaoishi
mbali na wapendwa wao na wale wanao pambana na hali hatarishi na gumu, katika kazi
yao baharini.
Mkutano katika Rome , unafanyika chini ya udhamini wa Rais wa
Baraza la Kipapa kwa ajili ya kazi za Kichungaji kwa Wahamiaji na watu wasiokuwa na
makazi maalum , Kardinali Antonio Maria VegliĆ² . Mkutano huu wa Wakurugenzi wa Mkoa
unajadili changamoto zinazo kabili Utume wa Kichungaji katika Mkoa wa Bahari.