2014-01-22 14:51:32

Papa kumpokea Rais Barak Obama Mach 2014.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya habari ya Vatican, Papa Francisko anatazamia kutembelewa Rais wa Marekani Barak Obama, Alhamisi Machi 27, 2014. Msemaji wa Vatican na Mkuu wa Ofisi ya Habari Vatican, Padre Federico Lombardi alieleza hilo siku ya Jumanne.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Obama kukutana na Papa Francisko, kutokana na kwamba, wakati wa Ibada ya Misa ya uzinduzi wa Utume wake kama Papa , Machi 19, 2013, Rais Barak Obama hakuhudhuria Ibada hiyo, badala yake aliwakilishwa na Makamu wa Rais wake Joe Biden.

Tangazo hili limetolewa zikiwa zimepita siku chache tu baada ya Katibu wa Nchi ya Vatican , Kardinali -mteule Pietro Parolin, kukutana na Katibu wa Nchi ya Marekani , John Kerry . Hata hivyo hiini safari ya pili Obaama kuwa Vatican, iMara ya kwanza, alimtembelea Papa Mstaafu Benedikto XVI, Julai 2009.

Katika ziara hii ya pili nchini Italia, Rais Baraka Obama pia atakutana na Rais Italia Giorgio Napolitano , na Waziri Mkuu wa Italia, Mheshimiwa Enrico Letta .Na ziara hii inatajwa kuwa sehemu ya ziara yake rasmi barani Ulaya, ambamo pia atatua katika mji wa The Hague March Machi 24 na 25 kwa ajili ya Mkutano utakao zungumzia usalama wa nuklia ulioandaliwa na serikali ya Uholanzi, katika mfululizo wa mikutano hiyo nchi humo.

Na Machi 26 Obama atakuwa Brussels Ubelgiji, kwa ajili ya mkutano wa kilele wa EU- US, pia kukutana na serikali ya Ubelgiji na kukutana na Anders Fogh Rasmussen , Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nato.







All the contents on this site are copyrighted ©.