2014-01-22 15:03:23

Papa asema , Mfarakano wa Makanisa ni kashfa



Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mahujaji na wageni Jumatano hii, imezungumzia Wiki ya Sala ya kuombea Umoja wa Kikristo, lililoanza Jumamosi iliyopita 18 Januari 2014 na litahitimishwa Jumamosi ya wiki hii , wakati wa Maadhimisho ya Siku Kuu ya Uongofu wa Mtume Paulo.
Papa amelitaja wiki hili kuwa ni juhudi za kiroho na ni wakati nyeti na maalum , unao unganisha Jumuiya za Kikristu kusali pamoja, juhudi zinazo fanyika kila mwaka kwa karibia kipindi cha karne moja . Pia ameutaja kwamba, ni wakati wa majitolea na maombi kwa ajili ya kuombea umoja wa wabatizwa, kama yalivyo kuwa mapenzi ya Kristo, ili kwamba, wote wawe wamoja (Yn 17:21). Kwa mwaka huu, wiki hili linaongozwa na Madambiu “Je Kristo amegawanyika? (1 Kor 1:13)”.

Papa anasema kwa hakika Kristo hajagawanyika. Lakini ni lazima kutambua tena kwa uchungu kwamba, jumuiya ya Kikristu inaendelea kuishi kwa kufarakana, na hii ni kashfa. Hakuna neno jingine linaloweza kutumika zaidi ya kuwa kashfa, Papa alisisitiza, na kuonyesha masikitiko yake kwamba , kama Mtume Paulo alivyo lionya kanisa la mwanzo hata leo hii bado kuna migawanyiko hiyo ya kusema, Mimi ni wa Paulo , Mimi ni wa Apolo , Mimi ni wa Kefa, au Mimi ni wa Kristo . Hata wale waliodai Kristo kuwa kiongozi wao Mkuu, Paulo hakuwapongeza kwa sabau walilitumia jina la Kristu kujitenga na wengine ndani ya jumuiya ya kikristo.
Lakini Jina la Kristu hujenga ushirika na umoja , na si mgawanyiko ! Kristu alituletea ushirika kati yetu, si kututenganisha. Ubatizo na Msalaba ni mambo muhimu kwa wafuasi wa Kristu katika usharika wao. Na hivyo migawanyiko hudhoofisha uaminifu na ufanisi wa ahadi yetu kwa ajili ya kazi za uinjilishaji na huleta hatari ya kudharirisha nguvu za Msalaba.

Papa alieleza na kurejea jinsi Mtume Paulo alivyo wakemea Wakorintho kwa migogoro yao , lakini pia alimshukuru Bwana " kwa neema ya Mungu iliyotolewa kwao katika Kristo Yesu, ili katika Yeye mnakuwa na utajiri zawadi zote za maneno na maarifa yote.
Papa anasema, ni vizuri kutambua neema hii ambayo Mungu anatubariki na hata zaidi , kupata Wakristo wengine wengi na kuwapokea kama zawadi.
Na hii zaidi ya yote inahitaji maombi mengi , inahitaji unyenyekevu, tafakari na uongofu thabiti. Papa ameomba nakuwahimiza Wakristu kusonga mbele katika barabara hii ya kuombea umoja wa wakristo , ili kashfa dhidi ya umoja wa Wakristu itokomezwe kabisa miongoni wam Wakristu.
Katika wiki hili la Sala ya kuombea Umoja wa Wakristu, kati ya waliofika kusikiliza katekesi ya Papa ni pamoja na wanafunzi kutoka Chuo cha Kiekumene cha Bossey. Na pia walikuwepo mahujaji kutoka Shirikisho la Wayahudi la Chicago








All the contents on this site are copyrighted ©.