2014-01-21 09:17:30

Kardinali ahimiza Wanasiasa Sudan Kusini kujenga amani na maridhiano


Askofu Mkuu Zuberi Kardinali Gabriel Wako wa Jimbo Kuu la Khartoum Sudan , ametoa ombi kwa viongozi wa kisiasa, Sudan Kusini, kuweka kando maslahi yao binafsi, wanapotafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa katika taifa lao changa la Sudan Kusini.
Kardinali Wako , alieleza hilo akiwa Juba, Mji Mkuu wa Sudan ya Kusini,ambako ana hudhuria Mkutano wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Sudan na Sudan Kusini. Ametoa wito kwa Sudan Kusini kutambua kwamba , binadamu wote ni wana wa Mungu , na hivyo kuu ni dhambi.
Mapambano kati ya viongozi waweili pinzani katika chama tawala cha SPLM ( Sudan Watu Liberation Movement ), Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar, kwa sasa yanaonekana kuwa na mwelekeo wa mgawanyiko wa kikabila, makabila mawili makubwa nchini Sudan Kusini, Wadinka na Wanuer .

Wakati huo huo, licha ya mazungumzo yanayoendelea Addis Ababa Ethiopia kati ya wawakilishi wa wapinzani hao wawili , vita inaendelea, hasa katika eneo la mji wa Malakal , Mji muu wa Jimbo la Upper Nile, ( kaskazini-mashariki ). Hapo Januari 18, jeshi liliweza kuchukua udhibiti wa Mji wa Bor , ambao ni Mji Mkuu wa Mkoa wa Jonglei (Mashariki). Mapigano haya hasa yanafanyika kAtika mikoa yenye utajiri mkubwa wa rasIlimali. Mapambano yalianza Desemba 15. Mkoa mwingine ulio katika vita hivi ni Mkoa wa UNITA ambao mji wake Mkuu ni Bentiu .

Kuna hofu kwamba, iwapo mapigano hayatasitishwa hivi karibuni, Sudan Kusini itazama katika dibwi la umwangaji wa damu na uharibifu wa kivita, utakaolazimu pia vikundi vingine vyenye silaha na kuvikundi vingine vya kikabilia kuingilia kati na hivyo kuwa ni maafa yasiyo elezeka. Mpaka sasa machafuko yanayoendelea yameingia katika mwelekeo wa kimataifa , baada ya jeshi la Uganda kujiunga na jeshi la Kiir wakati pia Kenya imepeleka kikosi chake kwa ajili ya kulinda raia wake wanaioshi na kufanya kazi Sudan kusini, Shirika la habari la Fides limetaarifu. .







All the contents on this site are copyrighted ©.