Jifunueni wazi kwa Injili na maajabu ya Mungu – Papa Francisko
Jumatatu , Baba Mtakatifu Francisko, alisema uhuru wa Mkristo hupatikana katika utulivu
wa kulisikiliza Neno la Mungu na kuliishi. Papa alieleza wakati akihubiri katika
Ibada ya Misa, asubuhi, katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, ndani ya Vatican.
Papa alisema daima ni lazima kuwa tayari kuupokea ujumbe wa injili na miujiza ya Mungu
aliyo ihifadhi kwa ajili yetu sisi.
Alisisitiza kwamba, Neno la Mungu ni hai,
lina nguvu kamili , na hutambua hisia za moyo , lakini katika kulipokea, kwanza
ni lazima kulipenda na kuwa tayari kulipokea kwa moyo wazi. Katika Mahubiri hayo,
Papa alionyesha umuhimu na haja ya kweli, katika kuupokea ujumbe wa injili kwamba,
inahitaji kujenga tabia ya usikivu na uwazi.
Na aliweka bayana kwamba, Injili
si , tu , hutuambia yale tunayotaka sisi kusikia, lakini ni hai na lina nguvu na ni
kamili. Neno la Mungu - aliendelea – hutolewa bila gharama yoyote, ni kamili na limejaa
mambo mengi ya kustajaabisha,kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa Maajabu , Mungu wa
Ufunuo.
Neno hili linatuhimiza kubadilika na kuwa watulivu.Lakini ni muhimu
kwanza kupata ufahamu wa kina , nini maana ya kujiingiza katika mambo mapya ya injili.
Na alionya dhidi ya kuwa wadadisi wa kupita kiasi, watu wa kupenda kuuuchakachua
ujumbe wa Injili hadi kuwa jambo tofauti na lengo la Mungu.
Papa Francisko
alileleza hayo akirejea masomo ya siku ya Jumatatu , ambamo Nabii Samweli, anamkaripia
Mfalme Sauli kwa kutotii sauti ya Bwana na kwa kujaribu kuhalalisha uasi wake kwa
kuufunika ulafi wake kwa ukarimu. Papa alisema ni muhimu kuwa na tulivu na moyo mtiifu
,wenye kusikiliza sauti ya Bwana, na kufanya kile anachoamuru, ili katika kumtii,
inakuwa ni kushiriki katika maisha na upendo wake.
Na hii aliendelea, linatuongoza
sisi katika kutafakari juu ya uhuru wa kweli wa Mkristu na maana ya utii wa Mkristu,
ambavyo vyote viwili , hupatikana katika neno la Mungu na katika ujasiri wa kweli
, wa kuwa wazi katika ujumbe wake.
Jumatatu , Baba Mtakatifu Francisko, alisema
uhuru wa Mkristo hupatikana katika utulivu wa kulisikiliza Neno la Mungu na kuliishi.
Papa alieleza wakati wa homilia yake ya Ibada ya Misa, asubuhi, katika Kanisa dogo
la Mtakatifu Marta, ndani ya Vatican. Papa alisema daima ni lazima kuwa tayari kuupokea
ujumbe wa injili na miujiza yake aliyo ihifadhi kwa ajili yetu sisi.
Alisisitiza
kwamba, Neno la Mungu ni hai na huwa na nguvu kamili , na hutambua hisia za moyo
, lakini kwanza ni lazima kuwa wazi katika kulipokea. Akiwahutubia walioshiriki katika
Ibada hiyo ya Misa, Papa yalionyesha umuhimu na haja ya kweli, katika kuupokea ujumbe
wa injili, katika kujenga tabia ya usikivu na uwazi.
Papa aliweka bayana kwamba,
Injili - si tu hutuambia yale tunayotaka sisi kusikia, lakini ni hai na lina nguvu
na ni kamili. Neno la Mungu - aliendelea – hutolewa bila gharama yoyote, ni kamili
na limejaa mambo mengi ya kustajaabisha,kwa sababu Mungu wetu ni Mungu wa Maajabu
, Mungu wa Ufunuo.
Neno hili linatuhimiza kubadilika na kuwa watulivu. Na ni
muhimu kwanza kupata ufahamu wa kina nini maana ya kujiingiza katika mambo mapya ya
injili. Na alionya dhidi ya kuwa wadadisi wa kupita kiasi, watu tunaopenda kuuuchakachua
ujumbe wa Injili hadi kuwa jambo tofauti na lengo la Mungu.
Papa Francisko
alileleza hayo akiarejea masomo ya siku ya Jumatatu , ambamo Nabii Samweli, anamkaripia
Mfalme Sauli kwa kutotii sauti ya Bwana na kwa kujaribu kuhalalisha uasi wake kwa
kuufunika ulafi wake kwa ukarimu. Papa alisema ni muhimu ni kuwa na tulivu na moyo
mtiifu , kusikiliza sauti ya Bwana, na kufanya kile anacho tuamrisha kufanya ili katika
kumtii, inakuwa ni kushiriki katika maisha na upendo wake. Na hii aliendelea,
inatuongoza sisi katika kutafakari juu ya uhuru wa kweli wa Mkristu na maana ya utii
wa Mkristu, vyote viwili , hupatikana katika neno la Mungu na katika ujasiri wa kweli
wa kuwa wazi katika ujumbe wake.