Jumapili, Papa Francisko alifanya ziara ya Kichungaji , katika Kanisa la Moyo Mtakatifu
wa Yesu la Roma , katika mtazamo wa adhimisho la 100 tangu Kanisa kuanzisha Siku
ya Kimataifa kwa ajili ya kujali hali ya Wahamiaji na Wakimbizi. Kanisa hilo,
ambalo pia lina hadhi ya Basilika, lililoko karibu na Kituo cha Kikuu Treni cha Kati,
jijini Roma , huendeshwa na Wamisionari WaSalesians ya Don Bosco, ambao huhudumia
kwa ukarimu wageni wanaoingia jijini Roma bila kuwa na makazi. Kituo hicho kina uwezo
wa kuhudumia hasa vijana wakimbizi wanapatao 400 wanaotaufuta hifadhi kutoka maeneo
yenye ghasia za mapigano ya kisiasa kama Somalia , Eritrea , Gambia, Cameroon, Ghana
, Congo , Ivory Coast, Afganistan , Iraq, Iran, Kurdistan, Misri , Syria , Sudan,
Pakistan na Uturuki .
Akiwa mahali hapo , Papa Francisko alitoa wito kwa Wakristo
katika kila hali ya maisha - na hasa watawa, kuionyesha dhahiri imani yao ya upendo
wa injili ambao ni kujali na kutoa msaada kwa wahitaji kama kipaumbele cha kwanza
katika kazi zao na katika kuishuhudia Injili kwenye maisha yao ya kawaida ya kila
siku. Kati ya huduma zinazotolewa katika Kanisa hili la Moyo Mtakatifu ni pamoja
kujifunza Kiitaliani, masomo ya Udreva wa magari , elimu ya msingi , elimu ya kompyuta
mafunzo ya kazi na mipango.
Ziara hii ya iliyochukua takribani muda wa saa
nne , Papa alikutana watoto na waamini wa Parokia katika ukumbi wa Basilica, kufanya
mkutano na wakimbizi, na pia kukutana na watu wasio na makazi , kubadilishana salamu
na familia ambazo zilikuwa na watoto walio batizwa kipindi cha mwaka uliopita , na
pia wenyeji wake katika Kanisa hilo, jumuiya Wasalesiani na vijana na hatimaye kuongoza
Ibada ya Misa.