Papa Francisko akutana na Mtawa Arturo, mkongwe wa miaka 101.
Siku ya Jumamosi jioni , Papa akiwa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, alimpokea
,mtawa Arturo Paoli, Mzee mwenye umri wa miaka 101, na kuwa na mazungumzo ya faraghani.
Inaelezwa Papa katika mazungumzo na Mtawa huyo wa Shirika la Ndugu wadogo wa Yesu,
walizumgumzia zaidi kazi zake katika maisha ya kidini na kijamii kwa ajili ya watu
maskini, nchini Italia na Amerika ya Kusini, ambapo ameitumia miaka 45 ya maisha
yake. Mtawa Arturo Paoli, kwa sasa anaishi katika nyumba ndogo ya Mtakatifu Charles
de Foucauld , iliyoko karibu na mji wa wake wa kuzaliwa wa Lucca . Wiki chache zilizopita
Paulo alionyesha waziwazi nia ya kutaka kukutana na Papa Francisko , na hivyo kukafanyika
mpango kwa mkongwe , aweze kukutana na Papa. Na walikutana na kuwa na mazunguzo kwa
takrbani dakika 40 katika hali ya utulivu na faragha.
Mkongwe Paoli aliishi
Amerika ya Kusini, Argentina kwa miaka 14 , tangu 1960 mpaka 1974, ambako alikutana
Padre Jorge Bergoglio, wakati ule akiwa Mkuu wa kanda kwa WaJesuits . Kisha aliondoka
Argentina, hadi Venezuela na kuhamishiwa Brazil 1985 katika Brazil hadi kurejea Italia
mwaka 2005.