Msipoteze matumaini katika uwepo wa dunia bora zaidi-Papa Francisko.
Jumapili , Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, katika kuiadhimisha
Siku ya Kanisa ya Wakimbizi na wahamiaji , alitoa himizo kwa wakimbizi kutopoteza
matumaini ya kuingia tena katika dunia bora zaidi . Aidha alitoa shukurani zake za
dhati kwa wote wanaojitolea kutetea ubinadamu.
Adhimisho la Siku ya Kanisa
ya Kimataifa kwa ajili ya Wakimbizi Duniani, huadhimishwa kila mwaka tarehe 19 Januari.
Kwa mwaka huu imeongozwa na Mada Mbiu: "Kuelekea Dunia Bora Zaidi". Hotuba ya Papa
alilenga katika kuwajali wanaoishi kwenye mazingira magumu akisema, upendo ni njia
pekee ya kushinda uovu na dhambi. Katika maelezo yake, mbele ya melfu ya mahujaji
na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa kanisa kuu la Mtakatifu Petro,
alirejea maneno ya Mwinjilishi Yohane Mbatazaji “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye
dhambi ya ulimwengu"akisema , Yohana Mbatizaji, anatambua Yesu alikuja duniani kwa
kazi moja tu , nayo ni kumweka mtu huru dhidi ya utumwa wa dhambi, na alitoa malipo
ya kifo cha msalabani, kumkomboa binadamu kutoka dhambi zake.
Kwa namna gani?
Kwa njia ya Upendo. Hakuna njia nyingine ya kuondokana na uovu na dhambi , lakini
kwa upendo unaoongoza katika kuipokea zawadi ya maisha ya majitolea kwa ajili ya
wengine. Hivyo Yesu , alibeba mateso yetu na maumivu yetu, kwa gharama ya kifo chake
juu ya msalaba.
Yeye ni kweli Kondoo wa Pasaka, aliyezama katika kilindi cha
dhambi zetu, na kututakatifusha. Mtu na Mungu kweli, aliye jipanga katika mstari
wa wenye dhambi ili abatizwe, ingawa hakuhitaji kufanya hivo. Lakini alifanya hivyo
ili kuudhihirishIa ulimwengu kwamba ni Mtu aliyetumwa na Mungu Baba ulimwenguni kama
kondoo wa dhabihu.
Papa alieleza leo hii inamaanisha nini kuwa wanafunzi wa
Yesu, Mwana-kondoo wa Mungu ,akisema kwamba ni kuuweka ubaya na dhambi kando kwa
kutumia nguvu upendo na unyenyekevu badala ya kiburi. Na badala ya majivuno ni kuhudumia.
Papa
alisisitiza , msikubali kubaki na ufahali wa mahekalu bandia yaliyojengwa katika vilele
vya mlima, lakini kuweni watu wapole na walio wazi katika kukaribisha na kupokea
wengine hasa wenye shida kama wakimbizi na wahamiaji.
Na baada ya sala ya
Malaika wa Bwana, Papa kwa namna yakipekee alipeleka salaam zake za mataishi mema
kwa wawakilishi wa jamii na makabila mbalimbali waliokuwa wamekusanyika katika uwanja
huo wa Mtakatifu Petro . Na aliwahakikishi kwamba, wako katika moyo wa Kanisa kwa
sababu Kanisa ni watu walio katika safari kuelekea Ufalme wa Mungu, ulioletwa na Yesu
Kristu kati yetu.
Mapema, Papa aliotoa Ujumbe kwa ajili ya adhimisho la
mwaka huu 2014 , unaongozwa na MaNdhari “ Wahamiaji na Wakimbizi kuelekea dunia bora
zaidii, uliochapishwa Agosti ya mwaka 2013. Katika ujumbe huo , ameaandika, mabadiliko
ya tabia kwa wahamiaji na wakimbizi yanahotaji kila mtu, kujiweka mbali na mitazamo
ya upinzani na hofu na aina zote za utamaduni wa kubaguana na kuelekea katika mitazamo
msingi juu ya utamaduni wa kukutana , utamaduni wenye uwezo wa kujenga maisha bora
zaidi, kwa haki na udugu.