2014-01-18 11:36:13

Simameni kidete kulinda na kutetea Injili ya Uhai


Baba Mtakatifu Francisko anaunga mkono maandamano yanayofanyika nchini Ufaransa kwa ajili ya kulinda na kutetea Injili ya Uhai. Hayo yamebainishwa na Askofu mkuu Luigi Ventura, Balozi wa Vatican nchini Ufaransa ambaye amemwelezea kwa kina na mapana juhudi za Kanisa pamoja na watu wenye mapenzi mema kutaka kuenzi tunu msingi za maisha ya ndoa na familia, dhidi ya utamaduni wa kifo unaokumbatia sera za utaoji mimba na hali ya kutojali mateso na mahangaiko ya wengine.

Baba Mtakatifu anawaalika Waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kukumbatia na kuenzi Injili ya Uhai. Changamoto hii pia imetolewa na Baba Mtakatifu Francisko, hivi karibuni alipokutana na kuzungumza na Mabalozi pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.