Tume ya Makardinali inayosimamia na kuratibu shughuli za Benki ya Vatican kuendelea
na kazi yake
Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Tume ya Makardinali inayosimamia na kuratibu
shughuli za Benki ya Vatican, IOR, ambayo kwa sasa inaundwa na Makardinali: Christoph
Schornborn, Thomas Christopher Collins, Jean Louis Tauran, Santos Abril y Castillos
na Kardinali mteule Pietro Parolin.