2014-01-16 08:55:01

Mshikamano wa upendo kwa familia zinazokabiliana na ukata na hali ngumu ya maisha nchini Angola


Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Angola, hivi karibuni limepokea msaada wa vifaa vya kufundishia na michezo kutoka kwa Kampuni ya Mafuta ya Uingereza, BP, kama sehemu ya mchakato wa kuchangia kampeni ya Caritas Angola kusaidia familia zenye uwezo mdogo ili kuwasomesha watoto wao pamoja na kuchangia gharama za shule.

Askofu Tirso Blanco, Rais wa Caritas Angola anasema kwamba, msaada huu umetolewa kwa wakati muafaka kwani kuna familia nyingi nchini Angola zinakabiliwa na ukata wa fedha na hali ngumu ya maisha kutokana na ukame ulioikumba Mikoa iliyoko Kusini mwa Angola.

Caritas inaendelea kuwahamasisha watu binafsi na makampuni kuonesha mshikamano wa upendo kwa watu wanaohitaji msaada wa hali na mali kwa wakati huu.







All the contents on this site are copyrighted ©.