2014-01-15 10:50:05

Watu 200 wamekufa maji Sudan ya Kusini


Zaidi ya watu 200 wamefariki dunia kwa kuzama kwenye Mto Nile, jumapili iliyopita wakati baadhi ya wananchi wa Sudan ya Kusini walipokuwa wanakimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea kupamba moto nchini humo. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba, kuna zaidi ya watu 350, 000 ambao hawana makazi kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan ya Kusini.

Watu waliofariki dunia, Jumapili iliyopita walikuwa wanatoka kwenye kitongoji cha Malakal, kilichoko Mkoa wa Upper Nile.







All the contents on this site are copyrighted ©.