2014-01-15 14:44:43

Salam na matashi mema kwa Monsinyo Georg Ratzinger kwa kutimiza Miaka 90 ya kuzaliwa!


Monsinyo Georg Ratzinger, tarehe 15 Januari 2014 amesherehekea Miaka 90 tangu alipozaliwa kwa Ibada ya Misa Takatifu na tamasha la muziki, lilioandaliwa kwenye Bustani za Vatican na kuhudhuriwa na wageni mbali mbali kutoka ndani na nje ya Vatican.

Hayo yamebainishwa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican. Itakumbukwa kwamba, Monsinyo Georg Ratzinger ni kaka yake mkubwa Papa mstaafu Benedikto wa kumi na sita. Mashangilio yote haya ni kwa jili ya kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa wema na ukarimu wake kwa ajili ya zawadi ya maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.