2014-01-15 11:46:44

Chama cha Wakatekumeni Wapya kukutana na Papa Francisko, mjini Vatican, tayari kutumwa kutangaza Injili ya Furaha!


Baba Mtakatifu Francisko, tarehe Mosi Februari 2014 anatarajiwa kukutana na Wanachama 10, 000 wa Chama cha Kitume cha Ukatekumeni Mpya mjini Vatican, kama mwanzo mpya kwa wanachama kumi na saba kutumwa kuwatangazia watu wa Mataifa, Injili ya Furaha sehemu mbali mbali za dunia.

Baba Mtakatifu atawaombea na kutuma Familia 75 zilizoamua kuacha yote kwa ajili ya kutangaza Injili ya Furaha, katika miji waliyopangiwa. Familia hizi zinaundwa na kundi la watu wanne. Kundi hili hadi wakati huu linatekeleza utume wake katika miji 52 duniani, kwa kuwa na idadi ya familia 230. Watakapokuwa wanakutana na Baba Mtakatifu Francisko, wadau kutoka mataifa mbali mbali wamealikwa kushiriki.







All the contents on this site are copyrighted ©.