Vatican na Cameroon watiliana sahihi mkataba wa ushirikiano
Serikali ya Cameroon, Jumatatu tarehe 13 Januari 2014 imetiliana sahihi mkataba na
Vatican unaolitambua Kanisa Katoliki nchini Cameroon kisheria. Askofu mkuu Piero Pioppo,
Balozi wa Vatican nchini Cameroon amoongoza ujumbe wa Vatican katika hafla hii na
ujumbe wa Serikali ya Cameroon umeongozwa na Bwana Pierre Moukoko Mbondjo, Waziri
wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Cameroon.
Mkataba
huu una vipengele tisa vinavyobainisha nidhamu ya mahusiano kati ya Kanisa na Serikali
ya Cameroon kwa kuhakikisha uhuru wa kila taasisi kwa ajili ya mafao na ustawi wa
wananchi wa Cameroon: kimaadili, kiroho na kiutu. Uhusiano huu unapania kuchochea
maendeleo ya mtu mzima: kiroho na kimwili, kwa pamoja wakitafuta mafao ya wengi.
Utekelezaji
wa mkataba huu umeanza kazi baada ya pande mbili hizi kutiliana sahihi, kwenye Makao
makuu ya Wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Yaoundè,
Cameroon.