Takwimu zinaonesha kwamba, kuna jumla ya nchi na mashirika ya kimataifa 180 yenye
uhusiano wa kidiplomasia na Vatican. Tarehe 22 Februari 2013, Vatican ilianzisha uhusiano
wa Kidplomasia na Sudan ya Kusini. Itakumbukwa kwamba, Vatican pia ina uhusiano wa
Kidiplomasia na Umoja wa Ulaya, Shirika la Kitume la Malta na uhusiano wa pekee na
Wananchi wa Palestina.
Vatican ina mwakilishi wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa
na pia ni mwanachama wa kudumu katika Mashirika mengine 7 yaliyoko chini ya mwamvuli
wa Umoja wa Mataifa. Vatican pia ni mtazamaji wa kudumu katika Mashirika 8 ya Kimataifa
na Mashirikisho 5 ya Kikanda. Itakumbukwa kwamba, tarehe 5 Desemba 2011, Vatican ilikubaliwa
kuwa ni Nchi wanachama wa Baraza la Kimataifa la Wahamiaji.