2014-01-10 09:18:51

Vita bado inarindima Sudan ya Kusini!


Licha ya juhudi za Jumuiya ya Kimataifa kuendeleza majadiliano kati ya viongozi wa machafuko ya kisiasa nchini Sudan ya Kusini, lakini bado watu wanaendelea kupoteza maisha yao kutokana na mashambulizi, na kwamba, kuna kundi la watu ambalo limepata majeraha ya risasi na wanaendelea kupata tiba katika eneo la Lui. Watu bado wanaendelea kuhofia usalama wa maisha yao kutokana na vita inayoendelea kurindima nchini humo!

Kikundi cha Madaktari wa Afrika, CUAMM, kinasema, kinaendelea kutoa huduma tiba, chakula na malazi kwa watu wasiokuwa na makazi maalum, waliofanikiwa kutembea hadi mji wa Minkamen. Kuna zaidi ya watu, 20, 000 wanahitaji msaada wa dharura. Hospitali ya Yirol na Lui kwa sasa ni muhimu sana katika utoaji wa tiba kwa waathirika wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan ya Kusini.







All the contents on this site are copyrighted ©.