Baba
Mtakatifu Francisko, mapema Ijumaa hii aliwahakikishia waamini kwamba, imani thabiti
ina uwezo wa kuyashinda malimwengu. Na ili wawena imani thabiti hadi kuyashinda ya
kidunia, Wakristu, wanahitaji kuwa na ujasiri wa kumtegemea Mungu katika kila jambo.
Lakini kwa bahati mbaya Kanisa limejaa wakristu wenye imani nusunusu, isiyokuwa na
makali ya kuyashinda maovu ya kidunia. Papa Francisko alieleza katika mahubiri yake
wakati akiongoza Ibada ya Misa mapema Asubuhi ya Ijumaa hii katika Kanisa dogo la
Mtakatifu Marta hapa Vatican. |