Papa kutembelea Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu- Roma
Papa Francisko, Jumapili ya Januari 19, 2014 , nyakati za mchana, ana mpango wa kutembelea
Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, iliyoko katika eneo la Castro Pretorio hapa Roma,
karibu na kituo kikuu cha Treni cha mjini Roma. Akiwa katika Parokia hiyo, inayoongozwa
na Wamisionari Wasalesian, Papa ataongoza Ibada ya Misa. Kanisa hilo la moyo
Mtakatifu wa Yesu lililojengwa na Mtakatifu John Bosco kwa niaba ya Papa Leo XIII
, kwa ukarimu wa michango ya waamini wa Kanisa Katoliki, liliwekwa wakfu na Vika wa
wakati ule Kardinali Lucido Parocchi Mei 14, 1887. Na Papa Benedict XV, 11februari,
1921, aliliinua katika heshima ya Basilica ndogo. Hii ni Parokia ya nne kutembelewa
na Papa Francisko tangu awe Askofu wa Jimbo la Roma, mwezi March mwaka jana. Alikwisha
tembelea Kanisa la Watakatifu Elizabeth na Zakaria Mei 26 , na Desemba 1 alitembelea
Parokia ya Mtakatifu Cyril wa Alexandria na Januari 6 katika Kanisa Mtakatifu Alfonsi
Maria de ' Liguori,ikiwa ni ziara ya faragha kwa ajili ya kujionea pango hai katika
mazingira halisi ya wakati wa kzaliwa Yesu Bethlehem.