2014-01-09 15:04:05

Papa amsalimia Padre mzee kuliko wote Italia - Vatican


Jumatano baada ya katekesi yake kwa mahujaji na wageni, Papa Francisko, akiwa katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, alisalimiana na Padre Don Alessandro De Sanctis , mwenye umri wa miaka 95 ya kuzaliwa na miaka 72 ya Upadre , anayeaminika kuwa ni Padre Mzee kuliko Mapadre wote wa Italia. Padre Alessandro de Sanctis ni Paroko wa Parokia ya Filey Frusinate .
Wakisalimiana, Papa Francisko alimtania Don Alessandro ambaye kwa kumtazama haonyeshi kuwa na umri mkubwa kiasi hicho, kwa kumwambia umeificha wapi miaka hii yote 95, naye Padre alijibu , Mtu Mtakatifu niombee, kumpatia Papa, barua iliyoandikwa kwa mkono wake mwenyewe na kalamu ya zamani ya wino.
Akizungumza na wanahabari baada ya kukutana na Papa , Don Alessandro alieleza kwamba , alikuwa na wasiwasi moyoni kwamba Papa ataondoka mahali hapo bila kumfikia na hivyo alianza kukata tamaa na hata haikuona tena maana ya kuandika barua hiyo kwa Papa. Kimyakimya alisali ili Bwana amjalie neema ya kutoa mkono wake wa tisa kwa Papa, katika maisha yake. Na Bwana aliitikia Ombi lake .
Na alionyesha kushangazwa na unyenyekevu wa Papa Francisko katika kukutana na watu , akisema kweli ni jambo jipya linalo vutia wengi.








All the contents on this site are copyrighted ©.