2014-01-08 09:21:34

Zaidi ya watu millioni mbili wanahitaji msaada wa dharura Afrika ya Kati!


Umoja wa Mataifa unasema kwamba, kuna watu millioni mbili wanaohitaji msaada wa dharura Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati, walioyakimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini humo.

Taarifa hii imetolewa na Bwana Jeffrey Feltman, mkurugenzi wa masuala ya kisiasa Umoja wa Mataifa, wakati alipokuwa anawasilisha taarifa yake kwenye Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa. Anasema, nusu ya wananchi wanaoishi Bangui, Mji mkuu wa Jamhuri ya watu wa Afrika ya kati wamelazimika kuyakimbia makazi yao! Watu wanahitaji msaada wa chakula, dawa na mavazi.







All the contents on this site are copyrighted ©.