Katiba nchini Tunisia kwa mara ya kwanza inaonesha usawa kati ya mwanaume na mwanamke
mbele ya sheria
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi za Kiarabu, Bunge la Tunisia limepitisha
mabadiliko ya kipengele cha Katiba kinachoruhusu usawa kati ya wanawake na wanaume
nchini humo mbele ya sheria bila ubaguzi. Kipengele hiki kinazungumzia haki sawa miongoni
mwa wananchi wa Tunisia.
Muafaka huu umefikiwa baada ya majadiliano ya kina
yaliyofanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kutaka yafanyike mabadiliko ya kipengele
kilichokuwa kinaonesha ubaguzi wa kijinsi dhidi ya wanawake.
Mabadiliko haya
yataanza kutumika, tarehe 14 Januari 2014, kama kielelezo cha kumbu kumbu ya kuanguka
kwa utawala wa Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia, yapata miaka mitatu iliyopita.
Huu ukawa ni mwanzo wa upepo wa mageuzi kwa nchi za Kiarabu! Katiba mpya inatoa haki
kwa wananchi kutoa mawazo yao, kupata habari na kwamba, adhabu ya kifo imefutwa.
Baadhi
ya vyama na mashirika ya kutetea haki msingi za binadamu yanasema kwamba, mabadiliko
ya katiba bado yanayotoa mwanya wa wageni kutengwa nchini Tunisia, hata kama mabadiliko
haya yanaonesha usawa kati ya mwanaume na mwanamke mbele ya sheria. Kanuni ya usawa
bila ya ubaguzi inapaswa kuzingatiwa hata kwa wageni wanaoishi nchini Tunisia, vinginevyo,
ubaguzi unaweza kujionesha kwa njia ya: rangi, dini na mwelekeo wa kisiasa anaofuata
mtu!