Baada ya Siku Kuu ya Noel, mwaka Mpya na Epifania, Jumatano hii, Baba Mtakatifu ameanza
utoaji wa Katekesi zake za Jumatano kwa mahujaji na wageni. Na aliifungua Katekezi
ya kwanza na maelezo kwamba, kwa mfululizo atatoa katekesi juu ya Sakramenti ya Ubatizo,
katika umuhimu wake, kama pia inavyotajwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican
kwamba, Kanisa lenyewe ni " sakramenti ", ishara iliyojaa neema, ambayo hufanya kazi
ya kuokoa ya Kristo, iendelee kuwepo hata sasa katika historia, kwa nguvu ya Roho
Mtakatifu. Alieleza na kuitaja Sakramenti ya Ubatizo kuwa ya kwanza katika sakramenti
saba za Kanisa , ubatizo wenye kutuwezesha kuzaliwa upya katika Kristo, na kutufanya
kuwa washiriki katika siri ya kifo chake na ufufuko wa Kristu, ukitupatia dhamana
ya msamaha wa dhambi na kutuweka sisi upya huru, kama watoto wa Mungu na washarika
wa Kanisa lake. Papa alieleza na kuwasisitizia waamini wasisahau zawadi kubwa
wanaoipata kwa kubatizwa. Ubatizo unaotubadili , na kutupa tumaini jipya kuu na kutuwezesha
sisi kuingia katika upendo wa Mungu wa kukomboa watu wote, na hasa maskini , ambao
wameivaa sura ya Kristo. Ubatizo wetu pia ametupa haki ya kushiriki katika kazi
ya Kanisa za uinjilishaji , kama wanafunzi , na pia kama wamisionari. Aliongeza,
wakati huu tukisherehekea sikukuu ya Ubatizo wa Bwana Jumapili hii, sote na tumwombe
Bwana awezeshe upya ndani mwetu kwa neema ya ubatizo wetu na pia kwa ndugu zetu
wote na wake kwa waume , kuwa kweli watoto wa Mungu na washiriki hai wa Miwli wake
ambalo ni Kanisa. Baadaya yakatekesi Papa alisalimia katika lugha mbalimbali
na kuwatakia furaha tele ya amani ya Bwana.