Cheo cha Monsinyori kutolewa baada ya umri wa miaka 65-Vatican
Sekretarieti ya Jimbo la Takatifu , Jumanne ilitoa tamko linaloonyesha mabadiliko
yaliyofanywa na Papa Francisko katika utoaji wa cheo cha Monsinyori. Katika barua
iliyopelekwa katika ofisi zote za uwakilishi na wajumbe wa Papa duniani kote, (Nunciatures)
, pia kwa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki kwamba, katika majimbo yote duniani, cheo
hicho cha heshima pekee cha Kikanisa, tangu sasa katika maana hiyo ya Monsinyori itakuwa
sawa na “Kasisi wa Kipapa “. Na kwamba cheo hicho kitatolewa tu kwa Mapadre waliofikisha
umri wa miaka 65. Pia Barua hiyo, inatoa ufafanuzi zaidi juu ya matumizi ya cheo
hiki cha monsinyori , katika baadhi ya ofisi muhimu za Kanisa, - ambapo matumizi ya
jina Monsinyori limekuwa ni mila na desturi , kwa mfano katika ofisi ya Askofu,
au Mwakilishi Mkuu wa Jimbo au Vika wa jimbo , katika hilo bado hakuna mabadiliko,
kama ilivyo pia katika walio kabidhiwa dhamana ya huduma na kazi katika Ofisi za
Curia ya Roma, Na Pia barua inaweka wazi kwamba wale wote ambao tayari wamekwisha
pewa jina hilo rasmi wataendelea kulitumia .Na pia tamko jipya halifanyi mabadiliko
kwa walei waliotunukiwa heshima hiyo na Papa . Mwisho barua hiyo , inasema, Papa
Paulo VI, mwaka 1968, alipunguza wingi wa watu waliokuwa wakitumia jina la cheo hiki
cha heshima katika Kanisa. Na hivyo maamuzi ya Papa Francisko yako katika muono huohuo
wa ndani , watumishi wa kanisa kubaki watu wa kawaida.