Papa afanya ziara fupi katika Parokia ya Mtakatifu Alfonso de Liguori - Roma
Jumatatu jioni, Papa Francisko alifanya ziara fupi katika Parokia ya Mtakatifu Alfonsi
de ' Liguori ambako mamia ya watu, walikuwa wakimsubiri kwa hamu. Pamoja nae alikuwepo
Vika wa Jimbo la Roma, Kardinali Agostino Vallini, Pia Askofu Guerino di Tora wa eneo
la Kaskazini mwa JImbo la Roma.
Katika Parokia hiyo, Baba Mtakatifu alitembelea
pango hai la Parokia hiyo ambalo lilionyesha hali halisi za wakati wa kuzaliwa Yesu
kama ilivyoandaliwa na wanaparokia, kukiwa na wasanii mbalimbali wapatao 200 .
Baada
ya kuwa na muda wa faragha katika sala na maombi ndani ya kanisa hilo, Papa Francisko
alisalimia mstari mrefu wa waumini wapatao 200, walio wakilisha wanaparokia, mbele
yao kukiwa na watoto na wagonjwa wa parokia hiyo.
Katika salaam zake za ujumla,
Papa alisema, wanauanza mwaka mpya wakiwa na Yesu nae atabaki nao, kuwashindia maovu
, na katika kuwafanya kuwa watu wa amani na sala . Pia Papa alitoa mwaliko kwa
waamini kusali kwa ajili ya watu wote na zaidi sana kwa ajili ya watoto wanaozaliwa
na kwa ajili ya wazee ambao ni hekima ya jamii.
Pamoja na watu wazima pia kuliandaliwa
kundi la watoto wapatao mia waliomkaribisha Papa na wimbo maarufu “Wewe unayeshuka
chini kutoka katika nyota”. Pia wakiwa na shada la kubwa la maua mekundu ya waridi.