2014-01-04 16:02:43

Salini kwa ajili ya kuombea amani Sudan ya Kusini!


Waamini na watu wote wenye mapenzi mema kutoka Sudan ya Kusini, wanaalikwa kwa namna ya pekee kufunga na kusali kwa ajili ya kuombea amani na ustawi wa Sudan ya Kusini hasa wakati huu ambapo nchi hii inakabiliwa na machafuko ya kisiasa ambayo yamepelekea watu wengi kupoteza maisha na wengine wengi kuyakimbia makazi yao kwa kuhofia usalama wa maisha!

Waamini wanaalikwa kusali hili kwamba, juhudi za kutafuta amani kwa njia ya majadiliano zinazoendelea huko Ethiopia ziweze kuzaa matunda yanayokusudiwa, yaani amani, ustawi na maendeleo ya wananchi wote wa Sudan ya Kusini.

Waamini wanaombwa mahali popote walipo, wajikusanye na kusali kwa ajili ya nia ya kumlilia Mwenyezi Mungu ili aweze kuwajalia wananchi wa Sudan ya Kusini amani ambayo waliitamani kwa miaka mingi, lakini kwa sasa inaonekana kana kwamba inaweza kutoweka na matokeo yake machafuko kutawala tena!







All the contents on this site are copyrighted ©.