2014-01-03 14:50:33

Mheshimiwa Padre Fèlicien Mwanama Galumbulula ateuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Luiza, DRC


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Lèonard Kasanda Lumembo, C.I.C.M wa Jimbo Katoliki la Luiza la kung'atuka kutoka madarakani kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401§ Ibara ya 1.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Fèlicien Mwanama Galumbulula, Jaalim wa Chuo Kikuu na Katibu Mwambata wa Baraza la Maaskofu Katoliki DRC kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Luiza, DRC. Askofu mteule Fèlicien Mwanama Galumbulula alizaliwa tarehe 26 Oktoba 1960. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi akapadrishwa tarehe 9 Agosti 1987.

Tangu wakati huo amefanya utume katika nyadhifa mbali mbali ndani na nje ya DRC. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Katibu Mwambata wa Baraza la Maaskofu Katoliki DRC.







All the contents on this site are copyrighted ©.