2014-01-02 10:18:48

Rais wa Italia "achonga" na Baba Mtakatifu kwa njia ya simu!


Rais Giorgio Napolitano wa Italia katika shamra shamra za Mwaka Mpya wa 2014 amempiga simu na kufanya mazungumzo na Baba Mtakatifu Francisko. Wametakiana kheri na baraka tele kwa Mwaka 2014, ili kwa pamoja waendelee kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wa Italia na Jumuiya ya Kimataifa katika ujumla wake.

Rais Napolitano katika salam zake za Mwaka Mpya kwa wananchi wa Italia, alimshukuru kwa namna ya pekee Baba Mtakatifu Francisko kwa changamoto za maisha na utume wa Kanisa nchini Italia. Naye Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, alimshukuru Rais Napolitano na wananchi wa Italia kwa ujumla wao na kuwatakia kheri na baraka kwa Mwaka 2014.







All the contents on this site are copyrighted ©.