2014-01-02 12:01:11

Askofu Emmanuel Obbo, A.J. ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tororo, Uganda


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung'atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Denis Kiwanuka wa Jimbo kuu la Tororo, Uganda kadiri ya sheria za Kanisa namba 401ยง Ibara ya 1.

Baba Mtakatifu amemteua Askofu Emmanuel Obbo kutoka Shirika la Mitume wa Yesu, kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tororo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mtarajiwa Emmanuel Obbo alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Soroti. Baba Mtakatifu amemteua pia kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Soroti.







All the contents on this site are copyrighted ©.