2014-01-01 11:28:36

Baraka kwa Mwaka Mpya 2014


".. Bwana akubarikie, na kukulinda. Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani.." (Hesabu 6:22-27).


Mwaka mpya 2014 umeanza. Tushukuru Mungu kama tuliuanza katika mazingira ya kanisani kwa Ibada au hata kwa sala fupi na familia zetu. Kuna waliouanza, kwa bahati mbaya katika bar au fukwe za bahari. Hujachelewa bado, fanya hima katika juma hili ufanye ibada fupi na familia yako ili uanze na Mungu Baba.

Waisraeli walitamani sana kuanza kila kitu kwa baraka. Na ndio maana Mungu alimpa Musa "formula" hii ya baraka ili kuzima kiu yao. Tuone umuhimu wa baraka katika Maisha yetu. Tusikurukupe kwa cho chote Mwaka huu. Tuwe na unyenyekevu
wa kuomba baraka. Omba misa kanisani kwa lo lote unalonuia kufanya. Usifanye kwa akili na karama yako tu. Ujue wazi, Bwana asipoujenga mji waujengao wafanya kazi bure.

Tuombe :

Baba twaingojea kwa hamu sana kila Baraka utakayotukirimia kwa Mwaka huu mpya 2014. Baba uwe faraja na kimbilio la kila mmoja ndani ya familia zetu, kazi zetu, watoto wetu na rafiki zetu. Nyoosha mkono wako kwa kila familia zetu.

Imeandaliwa na
Padre Beno Michael Kikudo
Jimbo kuu la Dar es Salaam.








All the contents on this site are copyrighted ©.