2013-12-30 10:33:03

Sala ya Papa Francisko kwa Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu


Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, katika Maadhimisho ya Sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu, Jumapili tarehe 29 Desemba 2013 akiwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu alisali sala maalum kwa ajili ya kuombea familia duniani:

Yesu, Maria na Yosefu, ndani mwenu tunatafakari mng’ao wa upendo wa kweli, tunawatumainia. Familia Takatifu ya Nazareti, zijalie familia zetu pia ziwe ni mahali pa sala, shule makini ya Injili na Makanisa madogo ya nyumbani.

Familia Takatifu ya Nazareti, tunakuomba kusiwepo tena matumizi ya nguvu, hali ya kujifunga na migawanyiko katika familia zetu; tunakuomba kwa ajili ya wale waliojeruhiwa na kukwazika, waweze mapema iwezekanavyo kufarijika na kuponywa.

Familia Takatifu ya Nazareti, tunakuomba kwa ajili ya Sinodi maalum ya Maaskofu, iamshe tena dhamiri ya kila mmoja kuhusu utakatifu na tabia ya familia, uzuri wake kadiri ya mpango wa Mungu. Yesu, Maria na Yosefu, sikiliza sala yetu na ututimizie. Amina.








All the contents on this site are copyrighted ©.