2013-12-30 12:09:43

Masifu ya Jioni kwa ajili ya Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne, tarehe 31 Desemba 2013 majira ya jioni, anatarajiwa kuongoza Masifu ya jioni kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu na kesha kwa ajili ya Siku ya 47 ya Kuombea Amani Duniani kwa Mwaka 2014, inayoongozwa na kauli mbiu "udugu ni msingi na njia ya amani."

Mara tu baada ya Masifu ya Jioni, kutafuatia Ibada ya Kuabudu Ekaristi Takatifu; Utenzi wa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Te Deum na baadaye, Baraka kuu kwa kufunga Mwaka 2013. Kanisa linamwelekea Yesu Kristo ili kumwabudu, kumshukuru na kumtukuza kwa wema na ukarimu wake!

Linamkimbilia kuomba huruma na msamaha kutokana na mapungufu ya Watoto wake waliotawanyika sehemu mbali mbali za dunia pamoja na kuomba baraka ya kuendelea kuwa na imani na matumaini kwa siku za usoni.







All the contents on this site are copyrighted ©.