2013-12-28 10:50:59

Zaidi ya wafuasi millioni 11 wako kwenye akaunti ya @Pontifex


Baba Mtakatifu Francisko katika akaunti yake kwenye mitandao ya kijamii ya twitter, hadi kufikia tarehe 27 Desemba 2013 mchana, alikuwa na zaidi ya wafuasi millioni kumi na moja; wengi wao ni wale wanaozungumza lugha ya Kihispania, Kiingereza na Kiitalia. Wanafuatia wale wanaotumia kugha ya Kireno, Kifaransa, Kilatini, Kipolandi na Kiarabu.

Baba Mtakatifu katika kipindi hiki cha Noeli, ujumbe wake umejikita katika Fumbo la Umwilisho; akiwakumbusha waamini kwamba, Noeli ni muda maalum ambao Neno wa Mungu aliyefanyika mwili anakuja kuwatembelea watu wake, changamoto ya kujenga mazingira ya kuweza kukutana binafsi na Yesu. Katika kipindi hiki cha Noeli ambamo kuna utamaduni wa kutembelea Pango la Mtoto Yesu, waamini wanaalikwa na Baba Mtakatifu kuwakumbuka na kuwaombea wale wote wanaoteseka na kudhulumiwa kutokana na imani yao.







All the contents on this site are copyrighted ©.