Jeshi la Serikali ya Nigeria na Boko Haram bado wanapimana nguvu!
Katika mkesha wa Noeli kumekuwepo na mapambano makali kati ya Jeshi la Serikali ya
Nigeria na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram, ambacho kwa miaka minne, kimekuwa kikiendesha
vitendo vya kigaidi nchini humo na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali
zao.
Mapambano ya silaha yamefanyika katika eneo ambalo limetangazwa kuwa ni
la hatari, yaani kwenye Majimbo ya: Borno, Yobe na Adamawa. Serikali ya Rais Goodluck
Jonathan imetangaza hali ya hatari Kaskazini mwa Nigeria hadi mwishoni mwa Mei, 2014.