Uwakilishi kutoka Parokia za Jimbo la Roma kuungana na Papa Francisko wakati wa Ibada
za Misa za asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta
Inatazamiwa tangu, January 2014 , Maparoko wa Parokia mbalimbali za jimbo la Roma,
watapewa taarifa kupitia Vika wa Jimbo la Roma, lini wanaweza kupeleka maombi ya kushiriki
katika Ibada, zinazo ongozwa na Papa , katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta, ndani
ya Vatican.
Kulingana na nafasi ya Kanisa, Maparoko wataandamana na kundi
dogo la wanaparokia wapatao 25. Na kwa kuwa si rahisi Papa kupata muda wa kutembelea
Parokia zote za Jimbo la Roma, ushiriki huu katika ibada za asubuhi, utawezesha wanaparokia
mbalimbali kukutana na Askofu wao , walau kukiwa na nafasi mwakilishi mmoja kutoka
kila Parokia.
Padre Fedrico Lombardi, Msemaji wa Vatican ,ameeleza kama kujibu
makala iliyoandikwa katika gazeti la Corriere della Sera toleo la tarehe 24 .12 .13,
iwapo makundi ya waamini wa Parokia za Jimbo la Rome wamealikwa kushiriki katika
Ibada za Misa inayongozwa na Papa majira ya asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu
Marta ndani ya vatican, amesema, hadi Sasa waliohudhuria katika ibada hizo ni makundi
maalum ya wafanyakazi wa Vatican.