2013-12-26 11:35:01

Mchakato wa kutafuta suluhu ya amani Sudan ya Kusini


Viongozi wa Serikali kutoka Kenya na Ethiopia, siku ya Alhamisi tarehe 26 Desemba 2013 wamewasili Juba, Sudan ya Kusini kama sehemu ya mchakato wa kutafuta suluhu ya amani katika vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Sudan ya Kusini.

Wakiwa nchini humo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri mkuu wa Ethiopia Bwana Hailemariam Desalegn wamekutana na kuzungumza na Rais Salva Kiir wa Sudan ya Kusini. Viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa wanawataka viongozi wa Sudan ya Kusini kusitisha vita na kuanza majadiliano ya amani. Rais Salva Kiir katika ujumbe wake wa Noeli anasema, yuko tayari kufanya majadiliano na wapinzani wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.