2013-12-24 08:33:25

Wazee wa Kanisa wakutana kutakiana kheri na baraka za Noeli kwa Mwaka 2013


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu jioni alikwenda kumtembelea Papa mstaafu Benedikto wa kumi na sita, ili kumpatia salam na matashi mema ya Siku kuu ya Noeli kwa Mwaka 2013. Papa mstaafu Benedikto XVI alimpokea kwa heshima na taadhima Baba Mtakatifu Franciko kwenye lango la kuingilia kwenye Makazi yake mapya ya Monasteri ya Mater Ecclesiae iliyoko mjini Vatican.

Kwa pamoja walikwenda kusali kwa kitambo kidogo kwenye Kikanisa na kufuatia mazungumzo ya faragha yaliyodumu kwa kitambo cha dakika thelathini. Baba Mtakatifu Francisko alipata pia fursa ya kusalimiana na "Familia" ya Papa mstaafu Benedikto XVI.







All the contents on this site are copyrighted ©.