Kagera yahimizwa kudumisha umoja na mshikano -Askofu Msaidizi Kilaini
Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba, amehimiza wakazi
wa Mkoa wa Kagera kuona umuhimu wa uvumilivu wa kidini, kwa ajili ya udumishaji amani
na maelewano, kama ambavyo siku zote Watanzania wamekuwa wakiishi , kutokana na watanzania
wengi kujenga roho bora imara, yenye uelewa mpana katika masuala ya kisiasa na kiutamaduni
. Pia ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanapata muda wa kutosha kutoa malezi kwa
watoto wao, ili watoto waweze kupata majiundo sahihi katika kuwa raia wema.
Askofu
Kilaini alitoa wito huo, Jumanne iliyopita, katika hotuba yake ya kumpongeza Askofu
Mstaafu wa Jimbo la Bukoba , Askofu Nestorius Timanywa (76) , ambaye amestaafu baada
ya kuliongoza Jimbo la Bukoba kwa miaka 39.Hotuba iliyonukuliwa na Allafrica.
Alisema
wakati wanasherehekea tukio hilo, ni muhimu kuzichukua sherehe hizi kama somo la kujifunza
kutoka Roho wa mstaafu, Askofu Timanywa, jinsi alivyoweza kuwaunganisha watu wa imani
mbalimbali za kidini, wakati wote wa utawala wake . Na ndivyo inavyotupasa kushikilia
na kutoruhusu kabisa dini kuwa kigezo za kuigawa jamii.
Mungu aliumba watu
wote sawa . Na hivyo tunapaswa kuhakikisha kwamba, tofauti za kidini hazitutenganishi
au kutugawa katika maisha ya kijamii ya kila siku. Askofu Kilaini alieleza na
kuongeza wakati uongozi wa Askofu Timanywa, mlizaliwa Maaskofu wengine watano waliowekwa
wakfu. Aliwataja Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga, Askofu Msaidizi Methodius
Kilaini wa Jimbo la Bukoba, Askofu Desiderius Rwoma wa Jimbo Bukoba , Askofu Almachius
Rweyongeza wa Jimbo la Kayanga - Karagwe Na Askofu Mkuu Novatus Rugambwa wa Jimbo
la Sao Tome na Principe.Na pia alitaja jinsi Askofu Timanywa alivyo shuhudia kuundwa
kwa majimbo mapya matatu , Geita, Bunda na Kayanga - Karagwe.
Askofu Timanywa
alizaliwa tarehe 7 Mei 1937 parokiani Mugana , wilayani Misenyi Kagera. Alipadrishwa
Desemba 11 , 1966 , wakati Kardinali Laurian Rugambwa, alipohamishiwa Dar es Salaam
kuwa Askofu Mkuu wake na Askofu Gervas Nkalanga alipofanywa kuwa Askofu wa Jimbo la
Bukoba, hadi alipostaafu kutokana na hali ya afya , na Askofu Nestory Timanwa kuchaguliwa
kuwa Askofu Februari 24, 1974. Mwaka 1992, Jimbo la Bukoba lilifanya sherehe ya kutimiza
miaka mia tangu ukatoliki kuingia katika eneo hilo.