2013-12-23 11:33:36

Baada ya ziara yake Moscow Kardinali Kurt Koch asema..


Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili Umoja wa Wakristu, hivi karibuni alikamilisha ziara yake Moscow, ambapo alikutana na Patriaki Krill wa Moscow na Urusi yote na viongozi wengine wa kanisa. .
Katika maelezo yake , Kardinali Kurt Koch, baada ya kukutana na viongozimbalimbali wa Kanisa la Kiotodosi la Moscow na Urusi yote, ameonyesha kufurahia uwepo wa matumaini zaidi katika juhudi za kujenga umoja wa Wakristu.

Katika ziara hii yasiku sita, mjini St Petersburg na Moscow, aliweza kukutana na wawakilishi mbalimbali wa Kanisa la Orthodox na Kanisa Katoliki. Kardinali pia alipokelewa na Patriaki Kirill, wa Upatriki wa Moscow na Urusi yote , na pia Askofu Mkuu HilariĆ³n , mwenyekiti wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje kwa Kanisa na Mahusiano ya Upatriarki , ambayo tarehe 12 Novemba , alikutana na kuwa na mazungumzo na Francis Papa , mjini Vatican .
Ziara hii aliifanya kwa mwaliko wa Askofu Mkuu Paolo Pezzi , wa Jimbo Kuu Katoliki, la Mama wa Mungu katika Moscow, kwa ajili ya kushiriki katika maadhimisho ya Yubile ya Kanisa la Mtakatifu Catherine ya Alexandria, la mjini St Petersburg, ambalo limetimiza miaka 250 ya uwepo wake

Kardinali Kurt Koch akizungumzia kukutana kwake na Patriaki Krill , amesema, hii ni mara ya pili, mara ya kwanza alikutana na Patriaki Kirill Machi 2011, na walijadiliana masuala mbalimbali yakujenga, hasa uhusiano kati ya Kanisa la Kiotodosi la Moscoa na Urusi yote na Kanisa Katoliki. Na pia walitathmini hali ilivyo katika mwendelezo wa mazungumzo katika nyanja ya kiteolojia, kati ya Makanisa haya mawili, na changamoto za jamii ya leo yenye kuwa na mabadiliko na jibu la kawaida linaloweza kutolewa na kanisa katika kukabiliana na changamoto hizi. Na pia walitazama hali ya kisiasa ya dunia ambamo mmejaa machafuko ya hapa na pale na walilenga hasa katika machafuko ya Syria na machafuko ya kujirudia mara kwa mara Mashariki ya kati.

Katika mazungumzo hayo, Patriaki Krill pia alionyesha kuufurahia Utawala wa Papa Francisko , hasa katika namna zake anazotumia kuliongoza Kanisa Katoliki la Ulimwengu. Na mkazo wake katika kujenga mahusiano ya karibu na watu maskini, lakini pia na kujali changamoto hasa zinazokabili hali ya familia, akiweka tumaini lake kwamba, Sinodi ya Maaskofu, ya mandhari ya familia, itaweza kusaidia kutoa majibu kwa matatizo mengi yanayozikabili familia. .









All the contents on this site are copyrighted ©.