2013-12-21 11:34:27

Ongozweni na Mwanga wa Mungu aliyefanyika mwili!


Wakati huu Mama Kanisa anapoendelea kufanya tafakari ya kina kuhusu Fumbo la Umwilisho, tayari kushiriki katika Siku kuu ya Noeli ambayo inabisha hodi mlangoni, Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anakumbusha kwamba, kipindi cha Majilio ni hija ya maisha ya kiroho kuelekea Bethlehemu.

Anawaalika kujiachilia mikononi mwa Mwenyezi Mungu ili waweze kuongozwa na Mwanga wa Mungu aliyefanyika mwili!







All the contents on this site are copyrighted ©.