Zikiwa zimebaki siku tatu, kuadhimisha tukio la Mama Bikira Maria kutuzalia Mtoto
Yesu , Emannuel, Mkombozi wa Dunia, inafaa kwa wakati huu kumtafakari Mwanamke, mama
mzazi, hadhi yake, wajibu wake na Kanisa lasema nini juu mwanamke mama mzazi. Ni
wazi kipindi cha Krismas, ni wakati wa hekaheka nyingi za katika jamii , na familia
pia. Nyuso nyingi huonekana kuwa na furaha, na pia ndani ya familia, huonekana
mshikamano zaidi, ambamo licha ya hamu ya kusubiri ibada ya kusisimua ya Mkesha wa
Noel, pia kihali kuna mengi yanayofanyika. Baba anawazia familia watavaa nini na
familia itasheheka vipi, wakati mama nae akilini mwake amememezwa na mahangaiko ya
maandalizi ya mapochopocho ya mezani, na jinsi gani atawezesha familia yake kupendeza
siku hiyo, hata kama hawana fedha za kununua nguo mpya , bado atajitahidi zile walizo
nazo kuziweka katika hali nzuri, atazifua na kuzipiga pasi na kweli wote watatoka
katika hali ya utanashati. . Pongezi kwa hayo. ili kuweza kushirikishana mawazo
vyema katika kujadili mada hii ya Mama, na awaalika tuunganishe uchambuzi wetu na
maoni yaliyo andikwa na Mwenye Heri Papa Yohane Paulo II, katika waraka wake juu
ya Hadhi ya Mwanamke” Muliers Dignitatem ”. Katika kipengere cha 18 cha waraka
huo, alisema, ”ili tuweze kuelewa maana ya kuwa mama (motherhood), ni lazima kwanza
zaidi ya yote , kujaribu kupata uelewa wa kina juu ya ukweli wa mtu binadamu kama
ilivyotajwa katika Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatican, kwamba Binadamu , awe mke au
mme, ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu kwa namna ya kipekee, kwa ajili yake Mwenyewe
Mungu. Baba wa Milele aliyeumba ulimwengu kwa azimio la hiari na la siri, lenye hekima
na wema , akamuinua binadamu hadi kumshirikisha uhai wake wa Kimungu. Na pindi wanadamu
wanapoanguka na kumwasi, hawaachi kabisa bali huwapatia siku zote misaada ya wokovu
kupitia imani kwa mwanae pekee Yesu Kristu, aliyemwilishwa na kuja kukaa kwetu, Yesu
Kristu Mkombozi.
“Binadamu ni kiumbe pekeee aliyejaliwa utashi , wa kujiamulia
mambo yake mwenyewe. Hata hivyo, pia binadamu huyu hawezi kujiona amekamilika bila
ya kuwa karibu wa binadamu mwingine, kama ambavyo ufafanuzi huu wa mtu unavyokwenda
sambamba na msingi wa ukweli wa Biblia, kuhusu uumbaji wa binadamu - mwanamume na
mwanamke - katika sura na mfano wa Mungu . Hii si tafsiri ya kinadharia, wala kuwa
kifungu cha maneno yaliyo nakiriwa kutoka mahali, lakini yanatoa maana halisi na
kweli, maana ya kuwa binadamu , na wakati huohuo ikisisitiza thamani ya zawadi ya
binafsi , zawadi ya utu wa mtu. Katika mtazamo huo wa mtu, tunaweza pia kupata kiini
cha maadili ya jamii au taifa, “ ethos " ambayo kwa pamoja na ukweli wa uumbaji, unakamilishwa
na kitabu cha agano jipya”.. Mwenye Heri Yohane Paulo II, anaendelea kufundisha
kwamba, Ukweli huu juu ya mtu, pia unafungua njia ya ufahamu kamili wa umama wa mwanamke,
kwamba umama ni matunda ya ndoa, muungano wa mwanamume na mwanamke, kama ilivyoelezwa
katika kitabu cha Biblia kwamba muungano huu wa wawili watakuwa mwili mmoja " (
Gn 2:24). Na hili linaturejesha kumwona mwanamke kama sehemu zawadi ya binafsi maalum,
na pia kama kielelezo cha upendo wa wawili wanaoungana na kuwa mwili mmoja , na kutimizwa
yale yaliyoandikwa katika kitabu kitakatifu cha Biblia.
Zawadi hii ya pande
mbili za watu kuungana na kuwa mtu mmoja kupitia sakramenti ya ndoa hufungua zawadi
ya maisha mapya, binadamu mpya , yaani mtoto , ambaye ni nakala ya wa wazazi wake
. Umama ina maana , tangu mwanzo wake ni majitoleo maalum kwa ajili ya kuleta mtu
mpya. Ni majitolea ya wazi ya mwanamke mwenyewe. Katika uwazi huu wa mke na mme
waliokuwa mwili mmoja , mimba hutungwa , na kuzaliwa mtoto. Na hapo mwanamke hugundua
mwenyewe thamani hii ya zawadi binafsi ya majitoleo katika upendo wa kina.
Zawadi
ya utayari wa ndani wa kumkubali mtoto na kumleta duniani,kupitia muungano wa ndoa.
Kulingana na Biblia, kutunga mimba na kuzaa binadamu mpya , ni tukio la hali ya juu
sana ambalo kama mwanamke alivyosema, Nimeleta binadamu mpya kwa msaada wa Bwana"
(Mwa 4:01 ) Haya ni maneno ya Eva , Mama wa viumbe wote. Yanaonyesha furaha ya mwanamke
na ufahamu wake wa kushiriki katika siri kubwa ya mwendelezo wa binadamu, kuendelea
kuumbwa kizazi na kizazi, kupitia muungano wa ndoa , katika nguvu ya ubunifu wa
Mungu !
Nani kama Mama ! Ni maneno yanayogusa mioyo ya watu wote
duniani, katika kumzungumzia mama mzazi. Pamoja na hali ya mwanamke katika kipindi
cha kati ya mimba na mtoto kuzaliwa katika njia ya kawaida , kimwili na kisaikolojia
humpitia mengi, ambayo kwa wakati huu yanaeleweka vyema zaidi kisayansi kuliko ilivyokuwa
siku za nyuma, uchambuzi yakinifu wa kisayansi unathibitisha kwamba , mwanamke
ameumbwa na asili ya kuwa mama. Na hivyo kutunga mimba kama matokeo ya muungano
wa ndoa na mtu mme, huenda sambamba na muundo wa kisaikolojia na mwili wa mwanawake
. Watafiti waliofanya uchunguzi juu ya ukweli hu, wanathibitisha kwa kusema, ebu
waweke watoto wadogo mchanganyiko wa kike na kiume pamoja , wape vitu mbalimbali vya
kuchezea, utaona kwamba watoto wa kike wanapendelea kuchezea vitu vya kimama zaidi
kuliko watoto wa kiume, ikionyesha asili ya umama kwa mwanamke.
Mwenye Heri
Yohane Paulo II katika waraka wake wa Mulieris dignitatem, anasema, "umama ni mahusiano
maalum ya muungano katika fumbo la maisha yanayoanza na kukua ndani ya tumbo la mwanamke
. Mama wakati wa kulea mimba, hujawa na fikira nyingi na mshangao wa kile kinachoendelea
ndani mwake, na katika mwanga wa matumaini ya kutoa maisha mpya duniani, hukubali
na kumpenda mtoto anayembeba ndani mwake kwa kipindi cha meizi tisa. Haya ni mapenzi
ya ajabu na ya kipekee". Ingawa wanaume pia hushiriki kwa namna moja au nyingine,
katika kulea mimba, , wanasaikolojia wanasema zaidi sana kwa mama ambaye katika kipindi
hiki hujifunza mengi katika kumjali binadamu mwingine, ambaye hata hajamwona kwa macho
yake na hivyo huunda moyo huu wa kimama. Na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican ,
ukitazama ushiriki wa mwanamke katika ukombozi wa binadamu umeandika kwamba , Mungu
wa huruma alitaka Umwilisho utanguliwe na ukubali wake yeye aliyeteuliwa tangu milele
awe mama , ili kama mwanamke alivyoshiriki kuileta mauti pia kadhalika asaidie kuuleta
uzima.
Hayo yamhusu kwa namna ya pekee Mama wa Yesu aliyeuzalia ulimwengu
uzima wenyewe. Hivyo Maria , kwa kulikubali Neno la Mungu amekuwa mama wa Yesu. Bikira
Maria kwa kipaji na dhima ya umama wa kimungu unamwunganisha na mwanaye Mkombozi,
na kwa neema zake na huduma za kipekee ameunganika pia katika undani wa Kanisa. Mama
wa Mungu anakuwa ni kielelezo cha Kanisa katika imani , mapendo na umoja kamili na
Kristo.
Na hivyo , Kanisa Katoliki , limeitolea tarehe Mosi Januari kila mwaka
kuwa siku ya kumuenzi Mama wa Mungu, ambayo pia ni Siku ya Kuombea amani duniani.
Kijamii pia, huadhimishwa Siku ya Mama, katika tarehe mbalimbali , mbayo
husherehekewa kwa heshima ya akina mama na kutoa shukrani kwao kwa kuvumilia shida
na taabu wanazo pambana nazo katika kulea mtoto. Historia ya maadhimisho ya Siku
ya Mama, imetambuliwa kwa namna ya kipekee tangu enzi za zama za fahali za Ugriki
ya kale na imedumu hadi leo hii. Na kwa sasa inasherehekwa kwa kishindo katika mataifa
zaidi ya 40 duniani kote.
Mfano nchini Marekani, Azimio la kuwa Siku ya kumuenzi
Mama lilitiwa saini na Rais wa Marekani Woodrow Wilson Mei 8, 1914, kuheshimu akina
mama na wanawake wajawazito, na ushawishi wa akina mama katika jamii. Ni siku ya
kumtafakati Mama mwalimu wa kwanza wa binadamu. Afrika Kusini Siku ya Mama husherehekewa
kitaifa kila Jumapili ya pèili ya mwezi Mei. Na huiadhmisha Siku hii kaika roho wa
kweli anayeonyesha kutambua umuhimu wa mama ktika maisha yakilamtoto na hivyo ni siku
ya kumshukuru mama kwa upendo wao usiokua na kipimo na kwa huduma yao zuri ya siku
zote katika maisha ya mtoto, hata kama mtoto amekuwa mtu mzima, mama ni mama , wala
hakuna wa kulingana nae.