2013-12-21 08:33:18

Jifunzeni kuwa na matumizi bora ya chakula!


Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuguswa na mahangaiko ya watu wanaoteseka na baa la njaa sehemu mbali mbali za dunia kwa kusema kwamba, matumizi bora ya chakula yanaweza kusaidia kuganga njaa kwa mamillioni ya watu, kuliko tabia ya sasa ya kuputa chakula, wakati ambapo kuna watu wanakufa kwa njaa!

Huu ni ujumbe wa video uliotolewa na Baba Mtakatifu kwa ajili ya kundi la watu wanaojihusisha na kukusanya kadi zilizotumika nchini Argentina. Anasema, hii ni kazi nzuri inayosaidia kutunza mazingira na inaweza pia kuwa ni mfano bora hata katika matumizi ya chakula! Kuna haja ya kubadili mitindo na mfumo wa maisha kwa kujenga na kuimarisha mshikamano wa upendo, kuliko tabia ya utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya jirani.

Tabia hii si tu kwamba, inajionesha katika vitu la hasha! Baba Mtakatifu anasema imeanza kuingia hata katika utu wa mtu; kwani mtu anathaminiwa tu pale anapozalisha na kutoa huduma, nje ya hapo si mali kitu! Watu wajifunze kuheshimu na kutunza chakula kwa ajili ya mafao ya wengine pia!







All the contents on this site are copyrighted ©.