2013-12-19 15:31:06

Waziri mkuu Ralph Gonzales akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 19 Desemba 2013 amekutana na kuzungumza na Bwana Ralph Everard Gonsalves, Waziri mkuu wa wa San Vincenzo na Grenadine. Baadaye Waziri mkuu amezungumza pia na Askofu mkuu Pietro Parolin katibu mkuu wa Vatican na ujumbe wake.

Katika mazungumzo baina ya viongozi hawa wawili, wamegusia umuhimu wa Jamii kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai na tunu msingi za maisha ya ndoa na familia; elimu ipewe kipaumbele cha pekee sanjari na majadiliano ya kidini, ili kudumisha haki na amani.

Viongozi hawa wameonesha nia yakutaka kudumisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili na kuendelea kushirikiana katika medani za Jumuiya Kimataifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.