2013-12-18 08:05:06

Shikamaneni kwa ajili ya kutafuta mafao na maendeleo ya watanzania wote!


Dr. James Msekelea Balozi wa Tanzania nchini Italia na mwakilishi wa Tanzania kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko mjini Roma, ameupongeza Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki Watanzania mjini Roma, kwa kuonesha uhai, umoja, mshikamano na demokrasia. RealAudioMP3 RealAudioMP3

Ni matumaini ya ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwamba, utaendelea kuboresha ushirikiano kwa ajili ya mafao na ustawi wa watanzania na Kanisa katika ujumla wake.

Amesema, umoja na mshikamano ni mambo muhimu sana katika kukabiliana na hali mbali mbali za maisha, hasa wanapokuwa ugenini. Amewataka watanzania wanaoishi diaspora kusaidiana kwa hali na mali pamoja na kufahamiana ili kubadilisha uzoefu na mang’amuzi ya maisha.

Jumapili iliyopita watanzania walimkumbuka na kumwombea Hayati Nelson Mandela, Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini aliyezikwa, Jumapili tarehe 15 Desemba 2013 huko Kijijini kwake Qunu.







All the contents on this site are copyrighted ©.