2013-12-17 15:07:04

Kheri na Baraka Papa Francisko kwa kutimiza miaka 77 ya kuzaliwa kwako!


Baraza la Maaskofu Katoliki Italia limemtumia ujumbe wa matashi mema Baba Mtakatifu Francisko anapoadhimisha kumbu kumbu ya kuzaliwa kwake. Wanamshukuru kwa kujitosa bila ya kujibakiza kuwashirikisha watu Injili ya Furaha inayojikita katika maisha na huruma ya Mungu, ili kufungua tena hija ya matumaini kwa wale waliokata tamaa!

Kanisa Katoliki nchini Italia linatambua na kuthamini mchango wake unaojionesha kwa njia ya ushuhuda wa maisha. Waamini pamoja na wachungaji wao wanamsindikiza kwa njia ya sala. Wanahidi kuendelea kutangaza Injili ya Furaha.

Wakati huo huo, kituo cha Televisheni cha Vatican kimemtakia salam na matashi mema Baba Mtakatifu Francisko kwa kuonesha picha maalum za matukio tangu alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki hadi alipoadhimisha siku yake ya kuzaliwa, akiwa amezungukwa na watoto wanaohudumiwa kwenye Zahanati ya Mtakatifu Martha iliyoko mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.