Baa la njaa linanyanyasa watu zaidi ya millioni 2 nchini Afrika ya Kati!
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa linasema kwamba, zaidi ya watu millioni
mbili wanaoishi Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati wanakabiliwa na baa la njaa, ikiwa
kama hatua madhubuti hazitachukuliwa na Jumuiya ya Kimataifa ili kunusuru maisha ya
watu hawa!
Hii inatokana na uwepo wa vita na kinzani za kijamii kwa takribani
mwaka mmoja zilizopelekea wananchi kujikuta wanayakimbia makazi na nchi yao. Inakadiriwa
kwamba, kiasi cha asilimia 40 cha idadi ya watu wanaoishi vijijini wanakabiliwa na
uhaba mkubwa wa chakula, ikilinganishwa na wale wanaoishi mjini.
Wakulima
wengi vijijini wanashindwa kutekeleza shughuli zao kwa kuhofia usalama wa maisha yao.