2013-12-16 12:19:19

Papa aridhia uteuzi wa Kardinali Marc Ouellet kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia uteuzi wa Kardinali Marc Ouellet kuendelea kuwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu pamoja na kufanya uteuzi wa baadhi ya wajumbe wapya na wale wa zamani kuendelea na nyadhifa zao.

Kati ya wajumbe wapya ni Kardinali Francisco Robles Ortega, Kardinali Donald William Wuer, Kardinali Rubèn Salazar Gomes, Kardinali Kurt Koch, Kardinali Joao Braz de Aviz. Wengine ni Askofu mkuu Pietro Parolin, Askofu mkuu Beniamino Stella, Askofu mkuu Lorenzo Baldisseri, Askofu mkuu Vincent Gerard Nichols, Askofu mkuu Paolo Rabitti, Askofu mkuu Gualtiero Bassetti pamoja na Askofu mkuu Felix Genn.







All the contents on this site are copyrighted ©.